Luinasia Elikunda Kombe’s research while affiliated with College of Business Education and other places

What is this page?


This page lists works of an author who doesn't have a ResearchGate profile or hasn't added the works to their profile yet. It is automatically generated from public (personal) data to further our legitimate goal of comprehensive and accurate scientific recordkeeping. If you are this author and want this page removed, please let us know.

Publications (7)


Michakato ya Kisintaksia ya Uundaji wa Sentensi Changamani za Kiswahili
  • Article

March 2025

·

2 Reads

·

1 Citation

Kioo cha Lugha

Sephania M. Kyungu

·

Luinasia E. Kombe

Makala hii inalenga kuchambua michakato ya kisintaksia ya uundaji wa sentensi changamani za Kiswahili kwa kubainisha namna kishazi kikuu na kishazi bebwa vinavyowekwa pamoja kuunda sentensi hizo. Ili kufanikisha lengo hilo, makala imeongozwa na Nadharia Rasmi ya Chomsky (1965). Data za makala hii ni sentensi changamani za Kiswahili ambazo zilikusanywa kwa njia ya usomaji wa matini kutoka katika riwaya na magazeti. Matini hizi ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu sahili. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa mkabala wa kitaamuli kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa kimaudhui. Makala hii imebaini kwamba kuna michakato mitatu inayotumika kuunda sentensi changamani ambayo ni uchopekaji, udondoshaji-chopezi na udondoshaji-chopezi hamishi. Kwa kutumia Nadharia Rasmi, imebainika kwamba kila mchakato una hatua zake katika kuunda sentensi changamani.


Uchanganuzi wa Kirai Kihusishi cha Kiswahili

December 2024

·

3 Reads

MULIKA

Makala haya yanajadili muundo wa kirai kihusishi cha Kiswahili kwa kutumia mkabala wa sarufi miundo virai. Yanatambua kategoria tano za virai katika Kiswahili: virai nomino, virai kitenzi, virai kivumishi, virai kielezi, na virai kihusishi. Wataalamu wa sarufi ya Kiswahili wamekuwa wakitumia mkabala huu kuelezea muundo wa kirai kihusishi, lakini wanatofautiana kuhusu vijenzi vinavyohusishwa, jambo linalosababisha ukosefu wa urari katika uchanganuzi. Lengo la makala haya ni kubainisha muundo wa kirai kihusishi cha Kiswahili, kueleza sifa zake za kimuundo, na kufafanua sababu za kiisimu zinazowafanya wataalamu kutofautiana kuhusu uchanganuzi wa vijenzi vya kirai kihusishi licha ya kutumia mkabala mmoja wa sarufi miundo virai. Data zilichambuliwa kwa mbinu ya uchambuzi wa matini na mbinu ya uchambuzi wa maudhui. Matokeo yanaonesha kuwa kirai kihusishi kinaundwa na kihusishi kama neno kuu na kirai nomino au kishazi tegemezi kama vijalizo vyake. Neno kuu la kirai hutawala vijalizo vyake na halisimami peke yake. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa tofauti za kiisimu zinazofanya wataalamu watofautiane kuhusu uchanganuzi wa vijenzi za kirai kihusishi zinatokana na athari za tafsiri kutoka Kiingereza na kutokuzingatia kanuni za miundo virai.


Ala za Kisintaksia katika Ufafanuzi wa Dhima za Viambajengo vya katika Lugha ya Kiswahili

September 2024

·

82 Reads

Jarida la Kiswahili

Makala hii inahusu ala za sintaksia na namna ambavyo zinaweza kutumika katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za lugha ya Kiswahili. Licha ya ufafanuzi wa kina uliofanywa kuhusu mada hii, bado kuna masuala ambayo hayako bayana au yana utata. Mathalani, kuna utata juu ya dhima za kisarufi za viambajengo vinavyotokea mara baada ya kitenzi. Haiko wazi iwapo kila kiambajengo kinachotokea katika nafasi hiyo ni yambwa au la. Kwa hiyo, makala hii inalenga kufafanua ala mbalimbali za kisintaksia na kueleza namna ala hizo zinavyoweza kutumika kufafanua dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za lugha ya Kiswahili ili kutatua utata unaoweza kujitokeza kuhusu dhima hizo. Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya hojaji pamoja na usaili na kuchambuliwa kwa kutumia misingi ya Sarufi Leksia Amilifu. Kwa ujumla, tumebaini kuwa kuna ala kuu tano za kisintaksia katika lugha ya Kiswahili. Ala hizo ni pamoja na ukategoria wa neno, viambajengo vya maneno, viambishi, vijineno maalumu na kiimbo. Ala hizi ndizo zinazowasaidia wanasintaksia kufafanua dhima mbalimbali za kisarufi kama vile kiima, yambwa, yambiwa, yambwaϴ, oblikyumahali na chagizo. Ala za kisintaksia ni nyenzo muhimu katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za Kiswahili.


Udondoshaji wa Vipashio katika Vichwa vya Magazeti ya Kiswahili
  • Article
  • Full-text available

December 2023

·

18 Reads

MULIKA

Uandishi wa magazeti umeonekana kuwa wa kipekee kwani hutumia mitindo mbalimbali ya uandishi ukiwamo udondoshaji wa vipashio. Tafiti zinaonesha kwamba, udondoshaji wa vipashio katika vichwa vya magazeti hufanyika kwa lengo maalumu. Mathalani, inaweza kuwa ni kwa lengo la uwekevu, kuleta hamasa na mguso kwa msomaji. Licha ya kudhihirika kwa mtindo huu, tafiti zilizochunguza udondoshaji katika magazeti ya Kiswahili zinataja kiambishi njeo pekee kama kipashio kinachodondoshwa katika uandishi wa vichwa vya magazeti ya Kiswahili. Aidha, tafiti tangulizi zinaonesha kuwa vipo vipashio vingine vinavyodondoshwa katika uandishi wa vichwa hivyo ambavyo vinaweza kuchunguzwa kwa mkabala wa kisintaksia. Hali hiyo imeibua ari ya kutaka kuchunguza udondoshaji wa vipashio hivyo na changamoto zake kwa wasomaji. Data za makala haya zilipatikana maktabani katika magazeti teule ya Kiswahili, yaani Mwananchi, Nipashe, Habari Leo na Uhuru kwa kutumia mbinu ya usomaji na uchambuzi wa matini. Data zilichambuliwa kwa kuzingatia mkabala wa kitaamuli wakiongozwa na Nadharia Rasmi ya Chomsky (1965). Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kwamba, vipashio vinavyodondoshwa katika uandishi wa vichwa vya magazeti ni visabiki vya vitenzi visoukomo, kiima cha sentensi tendwa, kiima cha sentensi tenda, vihusishi, viunganishi na vitenzi. Udondoshaji huu pamoja na kuonekana kama mtindo, vilevile wakati mwingine umeonekana kuwa na changamoto ya kuleta utata kwa msomaji.

Download

Dhima za Kipragmatiki za Kiunganishi na Baina ya Vishazi Ambatani katika Lugha ya Kiswahili

May 2023

·

125 Reads

Utafiti

Ikisiri Makala hii inalenga kufafanua dhima za kipragmatiki zinazodokezwa kwa kiunganishi ‘na’ baina ya vishazi ambatani katika lugha ya Kiswahili. Dhima hizo huonyesha mahusiano yaliyopo baina ya vishazi vilivyoambatanishwa kwa kiunganishi hicho. Makala hii inaongozwa na nadharia ya Uhusiano ya Sperber na Wilson ambayo inahusu utambuzi wa binadamu na mawasiliano. Data zilizotumika katika makala hii zimepatikana katika machapisho ya kifasihi, hotuba na magazeti. Makala imeonyesha kuwa kiunganishi ‘na’ kina dhima mbalimbali za kipragmatiki ambazo ni uongezi, usababishi, ukinzani, usambamba na ufafanuzi. Dhima hizo ni fasiri ya mahusiano yaliyopo baina ya vishazi ambatani ambayo hayakusemwa kwa uwazi. Makala imeonyesha kuwa kiunganishi ‘na’ ni kiashiria muhimu cha kiisimu kinachomwongoza mshiriki wa mazungumzo kupata fasiri iliyokusudiwa kwa kudhibiti mchakato wa ufahamu. Pia, makala imeonyesha kwamba kiunganishi ‘na’ hutumika sambamba na viashiria vingine vya kiisimu na vya kiulimwengu kuashiria fasiri mahususi iliyokusudiwa baina ya vishazi vilivyoambatanishwa.


Respondents' Characteristics in Pujon District
Insight and Standpoints of the Dairy Farmers in Pujon District
DAIRY FARMERS’ KNOWLEDGE AND STANDPOINTS REGARDING FORAGE PRESERVATION TECHNOLOGY IN “NEW NORMAL” ADAPTATION (A Case Study in Pujon District)

September 2022

·

14 Reads

Jurnal AGRISEP Kajian Masalah Sosial Ekonomi Pertanian dan Agribisnis

Covid-19 pandemic has restricted social and physical mobility, such as using a mask during outdoor activities, applying hand sanitizer, washing hands, and maintaining health by exercising and controlling body intake. These restrictions also have caused the termination of forage subsidy by the milk processing industries. The “new normal” era requires farmers to secure self-sufficient forage. This research aims to 1; analyze the characteristic situation of the respondents regarding forage preservation technology in “new normal” adaptation, 2; analyze the insight and standpoints of the dairy farmers regarding forage preservation technology in “new normal” adaptation. The researchers used the descriptive analysis method and obtained 50 respondents by purposive sampling in Pujon District. The results showed that 63.70% of the respondents are “moderately informed," and 61.45% have "moderate standpoints". In conclusion, so it was concluded that the level of knowledge about forage feed preservation technology affected the attitude of farmers in applying forage feed preservation technology. the forage preservation technology is well-established and applicable among the dairy farmers in Pujon District.


Ufasiri wa Mahusiano ya Uwakati Baina ya Vishazi Ambatani katika Lugha ya Kiswahili

February 2021

·

1 Read

·

1 Citation

JULACE Journal of the University of Namibia Language Centre

Apart from forms that make the temporal relation explicit in coordinate structure, such as temporal connectives and adverbial of time, language has different ways of signalling that relation without using those forms. This paper intends to analyse how temporal pragmatic relations signalled between clauses which are linked by the coordinator na ‘and’ in Kiswahili. The study relies on Relevance Theory (cf. Sperber & Wilson 1986, Wilson & Sperber 2004) which is human cognition and communication theory. Using data from literature publications, speeches, government reports, and magazines, this paper reveals that coordinator na ‘and’ does not express temporality between coordinated clauses, as opposed to and in the English language (cf. Carston 2002). The paper shows that temporality relation in Kiswahili is expressed by -ka- tense affix and ku- infinitive affix. Ikisiri Mbali na kuwapo kwa maumbo yanayobainisha mahusiano ya wakati kama vile viunganishi vya wakati na vielezi vya wakati, lugha zina namna nyingine anuwai za kudhihirisha mahusiano hayo bila kutumia maumbo hayo. Makala haya yanalenga kufafanua namna mahusiano ya kipragmatiki ya uwakati yanavyoashiriwa baina ya vishazi ambatani vilivyoambatanishwa kwa kiunganishi ambatanishi na pasipo matumizi ya vielezi vya wakati au viunganishi vya wakati katika lugha ya Kiswahili. Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Uhusiano (taz. Sperber & Wilson 1995, Wilson & Sperber 1993, 2004) ambayo ni nadharia ya utambuzi wa binadamu na mawasiliano. Data za utafiti huu zimepatikana katika machapisho ya fasihi, hotuba na ripoti za serikali na magazeti. Matokeo ya makala haya yanaonesha kuwa kiunganishi ambatanishi na hakina dhima ya kipragmatiki ya kuashiria mahusiano ya uwakati, baina ya vishazi ambatani kama ilivyo kwa kiunganishi ‘and’ katika Kiingereza (taz. Carston 2002). Badala yake mahusiano hayo katika lugha ya Kiswahili huashiriwa kwa kiambishi njeo -ka- na kiambishi kisoukomo ku-

Citations (2)


... Vipashio hivyo vinaweza kuwa ni sauti au silabi. Vilevile, baadhi ya vipashio katika sentensi hudondoshwa ili kuepuka uradidi wa vipashio hivyo katika muundo wa nje (Wesana-Chomi, 2017;Kombe, 2019;Kyungu, 2022). Udondoshaji kwenye magazeti unajitokeza zaidi katika vichwa vya habari. ...

Reference:

Udondoshaji wa Vipashio katika Vichwa vya Magazeti ya Kiswahili
Michakato ya Kisintaksia ya Uundaji wa Sentensi Changamani za Kiswahili
  • Citing Article
  • March 2025

Kioo cha Lugha

... Hata hivyo, tafiti tangulizi zinaonyesha kwamba matumizi ya kiunganishi hicho na baadhi ya dhima zake zinatofautiana kati ya lugha na lugha. Kwa mfano, kwa mujibu wa Narty (2018) na Amfo (2011), vibadala vya kiunganishi 'na' katika lugha ya Kiga na Kidangme zinazozungumzwa nchini Ghana vina dhima ya kuonyesha mahusiano ya uwakati baina ya vishazi ambatani, wakati Kombe (2020) alibaini kuwa mahusiano ya uwakati baina ya vishazi ambatani katika lugha ya Kiswahili hayawasilishwi na kiunganishi 'na' bali na kiambishi njeo -ka-na kiambishi kisoukomo -ku-. Hali hii inaonyesha kwamba, dhima za kipragmatiki za kiunganishi 'na' na vibadala vyake katika lugha mbalimbali huweza kutofautiana baina ya lugha na lugha. ...

Ufasiri wa Mahusiano ya Uwakati Baina ya Vishazi Ambatani katika Lugha ya Kiswahili
  • Citing Article
  • February 2021

JULACE Journal of the University of Namibia Language Centre